Home - Publications
Publications
Back To Publication List  
Citizen Budget- 2012
  322290
Downloaded   Viewed
Citizen Budget- 2012
Category: Booklets
Author: HakiElimu  |  Editor: Elizabeth Missokia
Publication Details
ISBN-13: 1231
Publisher:
Publication date: 2012
Pages: 8
Summary:
Bajeti ya mwananchi ni nini? Bajeti ya mwananchi ni bajeti iliyorahisishwa na ambayo imewekwa katika muundo unaomfanya mwananchi wa kawaida aweze kuelewa mambo muhimu ambayo serikali imeyapanga katika mwaka wa fedha: fedha zitakazotumika na vyanzo vya mapato. Ni haki ya kila mwananchi kufahamu bajeti ya taifa. Kwa nini tuwe na bajeti ya mwananchi? Ziko sababu kadhaa zinazosababisha wananchi wengi kuwa nyuma katika kujihusisha na masuala ya bajeti nchini Tanzania:‐ • Lugha inayotumika katika nyaraka za bajeti ni ya taaluma ya mahesabu, uchumi na takwimu ambayo ni ngumu kueleweka kwa mwananchi wa kawaida. • Wingi wa kurasa za nyaraka hizo huwatia uvivu wananchi wengi kusoma na kuelewa kilichomo. • Imani potofu; watendaji wengi serikalini na wananchi wenyewe huamini kuwa upangaji na uandaaji wa bajeti ni kazi inayowahusu wataalamu tu na wasomi wa taaluma zinazohusiana na hesabu na biashara. • Usiri; bado serikali inalifanya suala la bajeti kuwa ni la siri na hivyo kusababisha ugumu katika upatikanaji wa taarifa na nyaraka zinazohusu masuala ya bajeti.

  Swahili  
.pdf, 3.9 MB

Order This Publication
Contact Personal Detail