Home - Publications
Publications
Back To Publication List  
Ahadi za Serikali 2011/2012
  508780
Downloaded   Viewed
Ahadi za Serikali 2011/2012
Category: N/A
Author: HakiElimu  |  Editor: Elizabeth Missokia
Publication Details
ISBN-13: 21212
Publisher:
Publication date: 2012
Pages: 4
Summary:
Mwananchi, amka, fuatilia! Alipokuwa akitoa hotuba kwenye Chuo cha Ualimu Morogoro, mwaka 1966, Rais wa kwanza wa Tanzania aliwahi kusema, ‘Uongozi unaweza ukawa mzuri au mbaya, au usiojali, lakini kama watu wameamka na wanajitambua wenyewe, mienendo ya uongozi huo haiwezi kuendelea kupishana sana na mienendo na tabia ya jamii kwa muda mrefu.’ Kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere, wewe kama mwananchi unaweza kuiwajibisha serikali ukijitambua. Huu ni wajibu wako na ili uweze kuutekeleza kwa ufanisi, unahitaji pia kuujua wajibu wa serikali. Katika kuwezesha wananchi kutimiza wajibu wao, Shirika la HakiElimu limechapisha kipeperushi hiki, kinachoorodhesha baadhi ya kauli zilizotolewa na viongozi wetu kuhusu elimu. Kauli zilizochapishwa hapa ni zile zinazojumlisha ahadi za viongozi mbalimbali kufanya kitu fulani katika elimu. Baadhi ya mada zilizoongelewa ni madai ya walimu, upungufu wa maabara na umuhimu wa kujenga mabweni ya watoto wa kike wanaosoma sekondari. Ni wajibu wa wananchi kuuliza uongozi wao: utekelezaji wa ahadi hizi umefikia wap

  Swahili  
.pdf, 3.9 MB

Order This Publication
Contact Personal Detail