Home - Publications
Publications
Back To Publication List  
Ahadi za Serikali V
  513907
Downloaded   Viewed
Ahadi za Serikali V
Category: Others
Author: HakiElimu  |  Editor: Elizabeth Missokia
Publication Details
ISBN-13: 6767
Publisher: HakiElimu
Publication date: 2008
Pages: 12
Summary:
Huu ni mwaka wa nne wa serikali ya awamu ya nne ambayo kauli mbiu yake imekuwa ni �Maisha bora kwa kila Mtanzania�. Ahadi hii ilitolewa na serikali kwa Watanzania wakati ilipoingia madarakani mwaka 2005. Kama ilivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania, 2025 na MKUKUTA, moja ya malengo ya serikali ya awamu ya nne ni kuboresha na kuimarisha utawala bora ili kuleta maendeleo endelevu. Utawala bora una misingi yake, baadhi ya misingi hiyo ni pamoja na utawala wa sheria, uwajibikaji, uwazi, kuheshimu haki za binadamu, demokrasia, kupiga vita rushwa na ufi sadi na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala yanayowahusu.Kama sehemu ya kazi zake za uchechemzi, HakiElimu imekuwa ikifuatilia ahadi na maagizo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa serikali kupitia vyombo vya habari hususan magazeti. Ahadi na maagizo hayo hukusanywa pamoja na kisha kutayarisha kijitabu cha �Ahadi za Serikali�. Kijitabu hiki huonesha kiongozi aliyetoa ahadi, ahadi au agizo alilotoa na chombo cha habari ambacho ahadi au agizo hilo liliripotiwa. Lengo hasa la kutayarisha kijitabu hiki ni kuwataarifu wananchi kile ambacho serikali yao imewaahidi pamoja na kuwajengea uwezo wa wao kuiwajibisha serikali. Si hivyo tu, pia kijitabu hiki kinaweza kutumika kama zana ya kufanyia tathmini utendaji wa serikali na hivyo kuweza kupima uwezo wa serikali katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na ahadi inazotoa kwa wananchi wake.

  English  
.pdf, 133.9 KB

Order This Publication
Contact Personal Detail